Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Oktoba 5, 2022 amefanya uteuzi wa viongozi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar,Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi unaanza leo.

Mosi, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Hawwah Ibrahim Mbaye kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Udhibiti wa Mfumo wa Utoaji wa Leseni za Biashara, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo,Hawwah alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Leseni katika Baraza la Udhibiti wa Mifumo ya Utoaji Leseni Zanzibar.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua,Salmin Sharif Khatib kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara, Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,kabla ya uteuzi Salmin alikuwa Afisa Mipango Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Biashara, Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news