Rais Dkt.Mwinyi arejea nchini baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya siku nne nchini Oman

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, usiku wa Oktoba 14, 2022 akitokea nchini Oman baada ya kuhitimisha ziara yake ya Kikazi ya Siku Nne nchini humo.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuelezea mafanikio ya ziara yake ya kikazi ya siku nne nchini Oman. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar, akizungumzia mafanikio ya ziara yake ya kikazi nchini Oman, mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kulia kwa Rais ni Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzinar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohammed. (Picha na Ikulu).

Post a Comment

0 Comments