NA MWANDISHI WETU
KATIKA kukabiliana na magonjwa yasiambukiza, Uhuru FM kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasioambukiza Tanzania (TANCDA) wamezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na magonjwa yasioambukiza.


Chini ya mpango huo wa kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi zaidi ili kujikinga na magonjwa yasioambukiza, Meya wa Jiji la Dar es salaam, Kumbilamoto, ameiomba jamii kufanya mazoezi ili kujikinga ma magonjwa hayo ambayo yamekuwa ni tishio hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
Magonjwa yasioambukiza ni pamoja na Kisukari, Saratani, Kiharusi, maradhi ya Moyo, pamoja na Figo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Sidde, ameishukuru Uhuru Fm kwa kuwa na kampeni hiyo ambayo amesema itasaidia jamii kujenga tabia ya kufanya mazoezi ili kuweka miili yao sawa kiafya.

"Hii ni awamu ya pili ya Jogging ya Uhuru fm, ambapo awamu ya kwanza tulijikita zaidi katika masuala ya sensa ya watu na makazi 2022, ambayo kwa kiasi kikubwa tulifanukiwa, tukaona tusiishie hapo na sasa yaani leo tumezindua tena Jogging itakayojikita katika magonjwa yasiyoambukiza, tuhamasishe jamii ifanye mazoezi" alisema Ntiga.
Aidha, Ntiga amevishukuru vikundi mbalimbali vilivyojitokeza katika uzinduzi huo ikiwemo Jogging ya Vingunguti, Miembeni, Ukonga, pamoja na Tabata veteran.