Rais Samia ateua Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu wake

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 10, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhuru Yunus.

Mosi, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Dkt. Boniphace Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Luhende alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Dkt. Luhende anachukua nafasi ya Bwana Gabriel Paschal Malata ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Pili, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Bi. Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huu Bi. Mwaipopo alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bi. Mwaipopo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Luhende ambaye ametuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, uteuzi huu umeanza Oktoba 9, 2022.

Post a Comment

0 Comments