Serikali kutumia Bilioni 45/- ujenzi Barabara ya Ntendo hadi Muze mkoani Rukwa

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI inatarajia kutumia takribani Shilingi Bilioni 45 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Ntendo hadi Muze yenye urefu wa kilomita 25 kwa kiwango cha lami ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa,Mhandisi Nyamweru Fashe, kuhusu hatua ya ujenzi wa Daraja la Kisalala (m 35) lililopo katika barabara ya Laela – Mwimbi – Kizombwe (km 92), Mkoani Rukwa. (PICHA NA WUU).

Hayo yamesemwa mkoani Rukwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati akikagua mradi huo ulioanza kutekelezwa na unatarajiwa kutumia muda wa miezi 18 ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza kuwa uzalishaji wa mazao unakwenda sanjari na uboreshaji wa miundombinu ili kurahisisha bei na ufikaji wa haraka wa mazao kwa wateja.
Kazi za ujenzi wa Barabara ya Ntedo hadi Muze yenye urefu wa kilomita 25 inayojengwa kwa kiwango cha lami zikiendelea, Mkoani Rukwa.

“Mkoa huu unazalisha mazao mengi sana ambayo yanahitaji kufika kwa wakati kutoka eneo moja hadi jingine hivyo Serikali imeanza kujenga barabara hii kwa kilomita 25 lengo ni kuhakikisha gharama za usafirishaji zinapungua kupitia miundombinu wezeshi” amesisitiza Waziri Mbarawa.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Kisalala (m 35) lililopo katika barabara ya Laela – Mwimbi – Kizombwe (km 92) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 80, Mkoani Rukwa.

Waziri Prof. Mbarawa ameutaka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhakikisha inamsimamia kwa karibu Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kutoka kampuni ya China Geo Engineering Corporation ili ikamilike kwa viwango na kwa wakati.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Mhandisi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa, Suzana Peter, kuhusu hatua ya ujenzi wa barabara ya Ntendo (km 25) inayojengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani Rukwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya wa Sumbawanga, Sebastiani Waryuba, ameahidi kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi ili kuuwezesha mradi huo kukamilika na kuahidi kukamilisha taratibu za fidia kwa wale wananchi wanaodai na watalipwa kulingana na viwango vilivyowekwa kisheria.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa,Mhandisi Nyamweru Fashe, kuhusu eneo litakapojengwa Daraja la Kale (m 25), lililopo katika barabara ya Msishindwe hadi Mambwekenya (km 24) Mkoani Rukwa.

Mkuu wa Wilaya huyo ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu katika mkoa huo hali itakayorahisisha usafirishaji, kupunguza gharama na kuongeza pato kwa wananchi wa mkoa huo kupitia usafirishaji wa mazao.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa,Mhandisi Nyamweru Fashe, amesema mpaka sasa mradi umefikia asilimia sita na kwa sasa Mkandarasi anaendelea na kazi ya kukamilisha matabaka mbalimbali ya awali ya barabara.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja Mradi anayejenga Barabara ya Ntedo hadi Muze (km 25) Wang Tuquan, wakati Waziri huyo alipokagua mradi huo Mkoani Rukwa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mbarawa yuko Mkoani Rukwa kwa ziara ya siku moja ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Wizara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news