WAZIRI MKUU AENDA KOREA KUSINI KWA ZIARA YA KIKAZI

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo Jumapili, Oktoba 23, 2022 kwenda  jijini Seoul, Jamhuri ya Korea kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Akiwa Korea Kusini, Mheshimiwa Majaliwa atakutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa Han Duck-soo. Pia anatarajiwa kushiriki kongamano la biashara na kukutana na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda. Vilevile, atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini.

Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha mahusiano na Korea Kusini ambayo yamedumu kwa miaka 30. 

Vilevile, kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa bluu, utalii, mahusiano ya anga na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni.

Post a Comment

0 Comments