DIRAMAKINI yafanikisha kupatikana kwa mtoto BRAITON KAMFREDY MUJUNGU usiku huu akiwa hai

NA DIRAMAKINI

BABA mzazi wa mtoto BRAITON KAMFREDY MUJUNGU ameupongeza uogozi wa DIRAMAKINI  kwa kusaidia kusambaza kwa kasi taarifa za kupotea kwa mtoto wao huyo ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha na hatimaye kupatikana usiku wa kuamkia leo akiwa hai.
"Asante sana wana DIRAMAKINI kwa kuwezesha kusambaa kwa taarifa hii kwa haraka sana, hakika ninyi ni tunu ya Taifa... DIRAMAKINI, Mungu awabariki sana tena sana mkiongozwa na Bw.Godfrey Ismaely Nnko kwa kuhakikisha taarifa za blogu yenu zinasambaa kwa haraka na kuifikia Dunia na Watanzania kwa muda mfupi sana;

Baba mzazi wa mtoto BRAITON KAMFREDY MUJUNGU ameyasema hayo leo usiku wa Novemba 27,2022 baada ya mtoto wake kupatikana usiku wa kuamkia leo saa 12:33 akiwa hai.
Mbali na hayo amewapongeza Watanzania wote kwa sala na ushirikiano wao ukiwemo uongozi wa Serikali na chama Mtaa wa Msufuni Dovya kwa Mapunda Kata ya Chamanzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa kufanikisha zoezi hilo.

"WATANZANIA MUNGU AWABARIKI KWA SALA NA DUA ZENU MAANA HATUNA CHA KUWALIPA BALI MUNGU AWAZIDISHIE UPENDO DAIMA KWA WATANZANIA WOTE.
ASANTENI SANA TENA SANA,"ameeleza Baba mzazi wa mtoto BRAITON KAMFREDY MUJUNGU.

Post a Comment

0 Comments