Dodoma Jiji FC yawalambisha Coastal Union zabibu 1-0

NA DIRAMAKINI

VIJANA wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dodoma Jiji FC wameanza kuonesha makali yao baada ya awali kusalia mkiani katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Hasira zao wamezipeleka kwa wenyeji, Coastal Union ya jijini Tanga katika baada ya kuwabamiza bao 1-0.

Ni kupitia mtanange wa nguvu ambao umepigwa leo Novemba 30, 2022 katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Aliyesababisha kilio kwa Coasta Union alikuwa ni mchezaji wa zamani wa Coastal Union hiyo hiyo, Rashid Chambo dakika ya 90.

Mgeni na mwenyeji awali walionekana kucheza mpira wa kukamiana huku kila mmoja akitamani kuchomoka na ushindi, ambapo dakika 45 za kwanza zilikatika tasa.

Matokeo hayo yanaifanya Dodoma Jiji FC kufikisha alama 12 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya 13 Coastal Union inabaki na alama zake 12 pia za mechi 13 nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambayo ina timu 16, timu tano ambazo zipo kileleni kwa sasa vinara Yanga SC ndiyo namba moja ambao wanaongoza kwa alama 32 baada ya michezo 13, wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 32 baada ya michezo 14.

Simba SC inashika nafasi ya tatu kwa alama 31 baada ya michezo 14, nafasi ya nne inashikiliwa na Singida Big Stars FC kwa alama 24 baada ya michezo 13 huku nafasi ya tano ikishikiliwa na Geita Gold FC ambao ina alama 21 baada ya michezo 14.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news