Singida Big Stars yaondolewa adhabu ya kufungiwa kusajili

NA DIRAMAKINI

KAMATI ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeiodolea timu ya Singida Big Stars (SBS FC) adhabu ya kufungiwa kusajili.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 30, 2022 na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Bw.Cliford Mario Ndimbo.

Kwa mujibu wa Ndimbo, badala yake timu hiyo imepigwa faini ya shilingi mioni moja. "Faini hiyo inatakiwa kulipwa kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu.

"Uamuzi huo umefanywa leo na kamati baada ya kupitia hoja za SBS katika maombi yao ya marejeo (review) kuhusu uamuzi wa awali wa kufungiwa kusajili.

"Iwapo SBS haitalipa faini hiyo ndani ya muda uliowekwa, adhabu ya kufungiwa kusajili itabaki palepale,"imefafanua taarifa hiyo ya Ndimbo.

Post a Comment

0 Comments