Jahazi la Ihefu FC lazidi kuzama, Geita Gold FC yaikung'uta 1-0

NA DIRAMAKINI

WENYEJI wa Mabarali mkoani Mbeya, Ihefu FC wameendelea kujiweka katika mazingira hatari ya kusukumwa nje ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Ni baada ya kushindwa kutamba kwa Geita Gold kupitia mtanange ambao umepigwa Novemba 25, 2022 katika dimba la Nyankumbu mjini Geita.

Katika mtanange huo wa kuvutia, Geita Gold FC walipata bao la pekee kutoka kwa mshambuliaji wao, Juma Luizio dakika ya 41 akimalizia pasi ya kiungo Saido Ntibanzokiza.

Matokeo hayo yameifanya Geita Gold kufikisha alama 21 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya nne, wakati Ihefu inabaki na alama zake nane za mechi 13 sasa nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi hiyo ya timu 16 za Tanzania Bara.

Nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inashikiliwa na Yanga SC ya jijini Dar es Salaam kwa alama 29 baada ya kucheza mechi 11, nafasi ya pili ni Azam FC kwa alama 29 baada ya mechi 13.

Aidha, nafasi ya tatu inashikiliwa na Simba SC kwa alama 28 baada ya mechi 13, nafasi ya nne Geita Gold FC kwa alama 21 baada ya mechi 14 na nafasi ya tano ikichukuliwa na Singida Big Stars kwa alama 21 baada ya mechi 12.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news