Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF yaufungulia uwanja wa Kaitaba

NA DIRAMAKINI

KAMATI ya Leseni za Klabu (CLC) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeufungulia Uwanja wa Kaitaba uliopo mkoani Kagera baada ya kufanyiwa ukaguzi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 30, 2022 na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Bw.Cliford Mario Ndimbo.

"Kikao cha CLC kilichoketi hivi karibuni kilipitia taarifa ya ukaguzi ya uwanja huo ambao iliufungia kutokana na upungufu wa kikanuni, na baada ya kupitia taarifa ya wakaguzi wake kamati imeridhia uwanja huo kukidhi matakwa ya kikanuni, hivyo imeufungulia. Uamuzi huo wa CLC ni kwa mujibu wa Kanuni ya Leseni za Klabu,"imefafanua taarifa hiyo.

Wakati huo huo, klabu zote zimekumbushwa kuzingatia kanuni kwani CLC haitasita kuchukua hatua kwa klabu ambayo itakwenda kinyume.

Post a Comment

0 Comments