Mwakalebela apoteza matumaini Kimataifa

NA MWANDISHI WETU

ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredick Lameck Mwakalebela ameonekana kupoteza matumaini kabisa kwa klabu hiyo kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika kufuatia sare ya mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulipigwa jana dhidi ya Klabu ya Africain kutoka nchini Tunisia. 
 
Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam

Makamu huyo amesema kuwa, anafahamu jukumu lililopo mbele ni zito sana kwa wachezaji na Kocha Nasreddine Nabi watakapokua nchini Tunisia juma lijalo, lakini amewapa moyo wa kupambana ili kupata matokeo mazuri ambayo yataiwezesha timu kuingia hatua ya makundi.

Ikumbukwe pia Yanga SC ilitupwa nje na Al Hilal kwenye Kombe la Mabingwa barani Afrika baada ya kuruhusu bao 2-1, wakianzia nyumbani kwa suluhu ya 1-1, kisha mchezo wa marudiano kupata kipigo cha goli 1-0.

Mchezo wa mkondo wa pili unatarajiwa kupigwa mjini Tunis nchini Tunisia, Novemba 9,mwaka huu ikiwa ndio mchezo ambao umebeba hatima ya timu zote mbili ya kuingia hatua ya makundi.

Mwakalebela ameongezea kuwa, licha ya Klabu ya Yanga kutofanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa,uongozi wa Yanga unapaswa kuhamasisha ushindani wenye matokeo mazuri kwenye ligi ili kuepuka fedhea kutoka kwa watani wao Simba SC.

Sambamba na hili kampuni bora ya kubeti Tanzania Sokabet inakupa nafasi ya kuweka bashiri zako katika michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa,Casino, Zeppelin na virtual games.

Cha kufurahisha ni kuwa ushindi wake ni wa kibabe kutokana na ukubwa odds zake kwa kila mchezo na cha zaidi ni kuwa kila wiki Sokabet inatoa shilingi milion saba laki saba na elfu sabini na saba na mia saba sabini na saba,(7,777,777) kwa watu ishirini.

Wahi sasa, jisajili na weka bashiri zako kupitia Sokabet the Best Sports Betting in Tanzania  ili unufaike na bonusi pamoja na ushindi wa kishindo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news