Nyota 20 wa KMC FC kuwafuata Singida Big Star

NA DIRAMAKINI

KIKOSI cha KMC kesho kitaanza safari kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mchezo mwingine dhidi ya Singida Big Star utakaochezwa Novemba 23 saa 14:00 mchana katika Uwanja wa Liti mkoani humo.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni , itaondoka na wachezaji 20 ambapo kabla ya kuanza safari mapema asubuhi ya leo imefanya mazoezi ya mwisho kama sehemu ya kuendelea kujiweka sawa katika mchezo huo.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 20, 2022 na Christina Mwagala ambaye ni Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC.

KMC FC itakuwa ugenini ikiwa imetoka kupoteza mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Novemba 15 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na inakwenda Singida ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo muhimu ikiwa nyumbani.

Amesema, katika mchezo huo, timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Thierry Hitimana imejipanga kuhakikisha kwamba inafanya vizuri licha ya kuwa Singida Big Star ni timu nzuri ambayo pia inahitaji matokeo kutokana na kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

"Tunakwenda kupambana kwa mara nyingine ugenini, mchezo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani ambao tunakwenda kukutana nao pia wametoka kupoteza kama ilivyo kwetu, ila pamoja na ushindani huo KMC FC tuna wachezaji bora wenye uwezo mkubwa wa kuipambania timu kupata matokeo mazuri.

"Hakuna mchezo mwepesi , tunahitaji zaidi ushindi , wachezaji wote wapo imara na kila mmoja yupo tayari kuipambania Manispaa yetu ya Kinondoni , hatukuwa na wakati mzuri kwenye michezo miwili ambayo tulikuwa Kanda ya Ziwa, hivyo mashabiki zetu msiwe na hofu kwasababu siku zote timu bora huwa haipoteza mechi mara mbili,"amesema.

Kwa upande wa afya za wachezaji amesema, Matheo Anton ambaye hakuonekana kwenye michezo miwili tayari amerejea kikosini na wenzake, Awesu Ally Awesu ameanza mazoezi mepesi ya peke yake.

"Lakini pia tunaongezeko la wachezaji wawili wenye majereha ambao ni Emmanuel Mvuyekure pamoja na Kelvn Kijiri na kwasasa wanaendelea na matibabu,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news