Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wawili leo.

Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Sharifa Omar Salim kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma. Dkt.Sharifa ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 16, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said ambapo uteuzi huo wa Mheshimiwa Rais kwa viongozi hao unaanza leo.

Pili, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Hashim Hamza Chande kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Dkt.Hashim kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alikuwa Mkuu wa Skuli ya Kilimo, Kizimbani katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news