Rais Dkt.Mwinyi awaapisha watendaji mbalimbali wa Serikali

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi Novemba 11, 2022 amewapisha watendaji mbalimbali wa wizara za Serikali aliowateuwa hivi karibuni kushika nyadhifa zao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Abeda Rashid Abdallah kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,hafla ya kiapo imefanyika Novemba 11, 2022 katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa an viongozi mbalimbali wa kitaifa, akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalla, Dkt.Mwinyi amemuapisha Dkt.Islam Seif Salum kuwa Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais pamoja na Maryam Juma A. Sadalla kuwa Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Thabit Idarous Faina kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi, kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.

Aidha, amemuapisha Abeda Rashid Abdalla kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Maryam Juma A.Sadalla kuwa Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais,Kazi,Uchumi na Uwekezaji,kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt.Islam Seif Salum kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mkuu (kazi na uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais,Kazi,Uchumi na Uwekezaji,hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Khamis Abdulla Saidi kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Saleh Juma Mussa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu, kabla ya uteuzi alikuwa Afisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu,hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Viongozi wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama ni miongoni mwa waalikwa waliohudhuria katika hafla ya kiapo cha viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi hivi karibuni, katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman (kushoto), Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,pia Jaji Mkuu mstaafu Mhe.Hamid Mahmoud Hamid na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa wakiwa katika hafla ya kiapo kwa Viongozi walioteuliwa hivi karibuni, hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Katika hatua nyingine, Dkt.Mwinyi alimuapisha Saleh Juma Mussa kuwa Katibu Mkuu (OR) Ikulu, Khamis Abdalla Said kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, sambamba na Thabit Idarous Faina aliyemuapisha kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news