Yanga SC yatinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

NA DIRAMAKINI

YANGA SC ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara wametinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Ni baada ya kuichapa bao 1-0 wenyeji Club Africain kupitia mchezo uliopigwa katika dimba la Le stade olympique de Rad├Ęs jijini Tunis nchini Tunisia leo Novemba 9, 2022.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Yanga, Stephane Aziz Ki ndiye shujaa wa klabu hiyo ambapo akitokea benchi aliipatia bao muhimu timu yake dakika ya 79 akimalizia pasi ya Fiston Mayele.

Awali dakika 45 zilitamatika kwa timu zote mbili ubao kusoma sufuri, baada ya miamba hiyo kuoneshana soka la hali ya juu.

Katika mtanange huo, Kibwana Shomari ni miongoni mwa wazawa ambao wameonesha kiwango kizuri kwenye mchezo akiwa amepiga mashuti mawili ambayo yamelenga lango.

Post a Comment

0 Comments