Eden Hazard atangaza kutundika daruga

NA DIRAMAKINI

WINGA wa Ubelgiji, Eden Hazard siku ya Jumatano ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya miaka 14 ambayo ilitoa matokeo chanya uwanjani.

Picha na Bagu Blanco/PRESSIN.

"Ukurasa unageuka leo... Asante kwa upendo wenu. Asante kwa msaada wenu usio na kifani. Asante kwa furaha hii yote niliyoshiriki tangu 2008. Nimeamua kusitisha kazi yangu ya kimataifa, nitawakumbuka sana...,”Hazard amesema kupitia kwenye Instagram yake.

Tangazo lake lilikuja siku chache baada ya Ubelgiji kuondolewa katika hatua ya makundi katika Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) 2022 nchini Qatar.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye kwa sasa anachezea Real Madrid, alicheza mechi 126 za kimataifa na kuifungia Ubelgiji mabao 33.

Hazard alinyakua medali ya shaba katika Kombe la Dunia la FIFA la 2018 huku Ubelgiji ikimaliza mashindano hayo katika nafasi ya tatu.

Pia alishinda mataji ya ndani akiwa na Lille ya Ufaransa, Chelsea ya Uingereza na Real Madrid ya Uhispania, pamoja na Ligi ya Mabingwa ya UEFA akiwa na Real Madrid msimu uliopita. (Mashirika)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news