FIFA yakiri Qatar imevunja rekondi Kombe la Dunia 2022

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino ametaja Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) nchini Qatar 2022 kama bora zaidi kuwahi kutokea duniani.

Ni kufuatia mechi kali katika makundi yote nane, mahudhurio yaliyovunja rekodi na idadi ya watazamaji wa televisheni duniani kote.

Sambamba na Tamasha la Mashabiki wa FIFA huko Doha wakiwemo mashabiki wanaounga mkono mataifa kutoka kila kona ya Dunia.

Katika mahojiano yaliyochapishwa na tovuti rasmi ya FIFA, Infantino amesifu ubora wa soka unaohusisha timu 32 zilizoshiriki katika hatua ya makundi na akaangazia shauku iliyoonyeshwa kwenye viwanja, Tamasha la Mashabiki wa FIFA na viwanja vya mashabiki karibu na Qatar.

"Nimeona mechi zote, kwa kweli,nikiri wazi, hii imekuwa hatua bora ya makundi ya Kombe la Dunia la FIFA kuwahi kutokea. Kwa hivyo, inatia matumaini kwa muda uliosalia wa Kombe la Dunia.

"Mechi zimekuwa za ubora mzuri katika viwanja maridadi, tulijua hilo tayari.Vilevile, watu waliokuwa pale pia walikuwa wengi ajabu. Zaidi ya 51,000 kwa wastani,"amesema.

Infantino aliendelea kueleza kuwa, "Takwimu zimezovunja rekodi kwenye TV, tayari tulikuwa na watazamaji zaidi ya bilioni mbili, ambayo ni idadi ya kushangaza sana.

"Watu milioni mbili na nusu katika mji wa Doha na laki chache kila siku katika viwanja vya michezo, wote kwa pamoja, wakishangilia pamoja, wakiziunga mkono timu zao, mazingira mazuri, malengo makuu ni msisimko wa ajabu na mshangao.

"Hakuna tena timu ndogo na hakuna timu kubwa zaidi," Rais wa FIFA amesema. "Kiwango ni sawa sana. Kwa mara ya kwanza, pia timu za kitaifa kutoka mabara yote kuingia hatua ya mtoano, hii ni historia.

"Hii inaonnesha kuwa mpira wa miguu unazidi kuwa wa kimataifa. "Tunatarajia kuwa Kombe la Dunia la FIFA la Qatar 2022 litaendelea na kumalizika kama lilivyoanza kwa mafanikio ya ajabu. Nina hakika kwamba tutawafikia watazamaji bilioni tano kote ulimwenguni,” Rais Infantino amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news