Hoteli ya Mtume Mwamposa ya G7 Wonders Mbeya yawagusa viongozi, asema makubwa yanakuja

NA DIRAMAKINI

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson ameguswa na uwekezaji mkubwa wa hoteli ya kisasa uliotekelezwa na Mtume Boniface Mwamposa maarufu kama Bulldozer jijini Mbeya.
Mwamposa wa Huduma ya Inuka na Uangaze Tanzania (Arise and Shine Tanzania) amewekeza hoteli ya hadhi ya nyota tano jijini Mbeya ambayo inafahamika kama G7 WONDERS.
Dkt.Tulia Ackson ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Hoteli ya G7 WONDERS iliyofanyika Desemba 23, 2022 jijini Mbeya amesema, huo ni uwekezaji mkubwa na hata kila mmoja akiingia ndani ya hoteli hiyo hawezi kujutia.

Pia Dkt.Tulia alimuomba Mtume Mwamposa kuendelea kufanya uwekezaji wa namna hiyo katika maeneo mengine huku akiendelea pia kuzisaidia jamii zinazomzunguka.
"Tunayo mahitaji mengi, ya kiroho na ya kimwili sasa katika yale ya kimwili tunaomba uendelee kushirikiana hasa na jamii ambayo inakuzunguka, kwani jamii zina mahitaji mengi ya kimwili na kiroho.
Naye mmiliki wa hoteli hiyo ambaye pia ni mtumishi wa Mungu wa Huduma ya Inuka na Uangaze, Mtume Mwamposa alisema kuwa, uwekezaji huo ni mwendelezo wa mipango yake ya kuifikia jamii kubwa kiroho na kimwili.

"Tunafanya zaidi katika jina la Yesu. Vile vile siyo katika hili tu Mheshimiwa Spika, tuna mpango wa kuwa na shule hapa hapa Mbeya, hatutaki tuishie hapa, tayari Arusha tuna hospitali ambayo ni Kituo cha Afya,"amesema Mwamposa.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Juma Zuberi Homera alimpongeza Mtume Mwamposa kwa uwekezaji huo mkubwa ndani ya Mbeya ambayo ni fursa kubwa katika kutoa huduma na ajira kwa Watanzania wengi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

2 Comments

  1. Hotel, iko wapi hapa mbeya. Picha za hiyo hotel?, Ina hadhi ya nyota ngapi.

    ReplyDelete
  2. Hotel Local hamna hata namba za simu wala location wanaenda kibubu bubu

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news