Rais Dkt.Mwinyi:Tutoe wahitimu wenye uwezo wa kuhimili ushindani uliopo kwenye soko la ajira

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inaongeza jitihada za kukiendeleza Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kuwa chuo bora zaidi katika kuwaandaa vijana wenye umahiri na weledi kitaaluma na ubunifu wa kuzitambua fursa na kuzitumia ipasavyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Teknolojia ya Habari (Bachelor Degree of Information Technology Application and Management) wakati wa hafla ya Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika katika ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja, Desemba 28, 2022 na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe.Leila Mohammed Mussa.(Picha na Ikulu).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo kwenye mahafali ya 18 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Tunguu, Mkoa wa kusini Unguja, Desemba 28, 2022.

Dkt. Mwinyi amesema kuongezeka kwa idadi kubwa ya wahitimu waliofaulu masomo ya fani mbalimbali chuoni hapo ni hatua za maendeleo zilizofikiwa na chuo hicho.
Pia amesema, kwa mwaka huu 2022 idadi ya wahitimu imeongezeka kufikia 1913 ikilinganioshwa na 1894 waliohitimu mwaka jana hatua aliyoipongeza kwa tasisi ya elimu ya juu SUZA kwa mafanikio ya kuzalisha wasomi wa fani mbalimbali ambazo alizitaja kuwa ni nguvu kazi na chachu ya kusukuma mbele maendeleo ya Zanzibar.

Wakati huo huo, Dkt. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwapongeza wahitimu kwa hatua waliyofikia sambamba na kuwashauri kuitumia vyema elimu waliyoipata hapo kwa munufaa yao na taifa kwa ujumla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili (Doctor of Philosophy in Kiswahili), Nunuu Abdalla Mohammed, wakati wa hafla ya Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.

“Nachukua fursa hii kuwapongezeni kwa mafanikio hayo ya kitaaluma ambayo chuo chetu kinaendelea kuyapata,”alipongeza Dkt.Mwinyi.

Akizungumzia suala la ushirikiano baina ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na taasisi nyingine za elimu ya juu za ndani na nje, ikiwemo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na wadau wengine wa Elimu, Dkt. Mwinyi alieleza hatua hiyo itafanikisha azma ya kuleta mageuzi katika sekta ya elimu kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu.
“Tutoe wahitimu wenye uwezo wa kuhimili ushindani uliopo kwenye soko la ajira kwa kutumia elimu walioyoipata” alisema Dkt. Mwinyi.

Aidha, alikishauri chuo hicho kuzipatia ufumbuzi wa haraka changamoto zinazopitia ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Hata hivyo, Dkt. Mwinyi alieleza kuwa serikali inaendelea kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na chuo hicho kwa kuwapatia misaada ya hali na mali kwa kadri hali inavyoruhusu.

“Hata hivyo, bado naendelea kusisitiza haja ya kutafuta njia mbadala za kupata fedha ikiwemo kuchukua mikopo na kuanzisha miradi ya maendeleo itakayoleta faida kwa chuo,” alieleza Dkt. Mwinyi.
Kuhusu suala la uhaba wa rasilimali watu unaokikabili chuo hivyo, Rais Dkt. Mwinyi alieleza haja ya serikali kuajiri watumishi ili kuongeza nguvu katika taasisi za elimu za elimu ya juu wakiwemo wahadhiri, wakutubi na wataalamu wa maabara na watumishi wa fani ili kukidhi viwango vya ubora wa elimu ya juu nchini sambamba na kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi.

Akizungumza kwenye mahafali hayo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Mohamed Mussa, alisema juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kutoa vijana wasomi watakaokuwa na uwezo wa kujiajiri na kuzikimbilia fursa ili kupunguza msongo mkubwa kwa seikali na wazazi.
Alisema, jitihada za Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) ni kuzaliwa wasomi watakaochochea maendeleo chanya nchini.
Baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano wakati wa sherehe za Mahafali ya 18 yaliyofanyika katika ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,ambapo Mgeni alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Makamu mkuu wa chuo hicho, Prof. Moh’d Makame Haji alisema chuo kina mpango wa kujenga jengo la sayansi ya bahari lenye nia ya kuendeleza dhana ya Uchumi wa Bluu nchini ambalo alilieleza kwamba fedha zake tayari zimeidhinishwa na serikali.
Wahitimu wa Stashahada ya Tehama na Uhasibu (Diploma in Information Technology with Accounting) kwa mwaka wa masomo 2021/2022 walipotunukiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika sherehe za mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Dkt.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Cheti cha Sayansi ya Kompyuta 2021/2022 pamoja na fedha shilingi laki mbili, Hisham Mdungi Makame katika sherehe za mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Dkt.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Stashahada ya Afisa Tabibu 2021/2022 pamoja na fedha shilingi laki tatu, Ummul-Khayr Sadri Adulla katika sherehe za mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Dkt.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Shahada ya Afya na Mazingira 2021/2022 pamoja na fedha shilingi laki tano, Rainhulf G.Mfuse katika sherehe za mahfali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA ) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Dkt.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news