SERIKALI YATOA TAARIFA YA UHAKIKI NA UHUISHAJI WA VYETI VYA USAJILI WA TAASISI ZA KIDINI KUANZIA DESEMBA 12 HADI 19, 2022 KANDA YA KASKAZINI

NA DIRAMAKINI

OFISI ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema inaendelea na zoezi la uhakiki na uhuishaji wa vyeti vya usajili wa taasisi za dini zilizopo Kanda ya Kaskazini inayohusisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara kuanzia Desemba 12 hadi Desemba 19, 2022.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2022 na Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Wizara ya Ndani ya Nchi imefafanua kuwa, viongozi wa taasisi za dini wanapaswa kufika kwenye Kituo cha Uhakiki na Kuhuisha Vyeti vya Usajili wa taasisi zao kitakachokuwa katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news