Shirika la Reli Tanzania (TRC) laongeza mabehewa mapya 22 kuongeza ufanisi

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limeanza kufanya majaribio ya mabehewa mapya 22 yaliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya reli ya kati na Kaskazini ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake kwa wananchi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa shirika hilo, Jamila Mbarouk.

Bi.Mbarouk amesema kuwa,majaribio ya mabehewa hayo yameanza kwa kuyasafirisha umbali wa kilomita 400 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro huku ukiwepo pia mpango wa kuyafanyia majaribio kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma na Arusha.

Post a Comment

0 Comments