Waziri Kairuki atoa agizo TARURA kuhusu daraja lililokatika la Makanya kuelekea Suji

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amewaelekeza wataalamu wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro kufika kwenye daraja lililokatika la Makanya-Suji ili kuona ni hatua gani ya haraka inaweza kuchukuliwa liweze kurejesha mawasiliano ya eneo hilo.
Ametoa agizo hilo wakati akiwasimika Machifu wa Kipare kwenye hafla iliyofanyika kwenye Kata ya Suji wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Agizo la Waziri Kairuki limetokana na wananchi kuelezea adha wanayoipata baada ya kuvunjika kwa daraja hilo.

Mwananchi wa Kijiji cha Suji, Gurisha Mchome amesema, wakati wa mvua inabidi watembee mpaka Makanya ambapo kuna njia ya kupandisha mpaka kufika Suji tofauti na wakati daraja hilo halijakatika walikua wanatumia muda mfupi kufika Suji.
Daraja la Makanya-Suji lilikatika wakati wa mvua za vuli za mwaka 2021 na kupelekea adha kwa wananchi wa eneo la Suji wanaolazimika kutumia njia ambayo si rafiki msimu wa mvua kutokana na kujaa maji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news