Waziri Simbachawene ahimiza wananchi kutunza mazingira

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene amehimiza wananchi kuendelea kulinda na kutunza mazingira na kuhifadhi maeneo ya vyanzo vya maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipotembelea zahanati ya Winza.

Kauli hiyo imetolewa katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Kijiji cha Mkoleko Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Tuanzishe mradi wetu wa maji kupitia vyanzo vya maji tulivyonavyo kwenye Mlima, ili tupate maji ya uhakika kwa ajili ya shughuli za kijamii.”

Aidha, watendaji wa kata muendelee kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi ,ikiwa ni sambamba na kutunga sheria ndogo ndogo ili kuzuia ukataji wa miti katika kingo za makorongo ili kuzuia mmonyoko.

“Kama una miti pembezoni mwa shamba lako iache usiikate ili iendele kuzuia mmonyoko wa ardhi, inayoharibu miundo mbinu ya barabara.”
Waziri Simbachawene ameahidi kuendelea kuimarisha barabara zinazounganisha vijiji vyote vinavyounganisha kata ya Mansa kwa kuhakikisha barabara hizo zinafanyiwa ukarabati katika maeneo korofi.

Akimkaribisha Waziri, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa, Mhe. Richard Maponda amemshukuru Waziri Simbachawene kwa jitihada zake za kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Mpwapa, kuna zahanati sita zimefunguliwa na watu wanapata dawa.

“Kuna shule zimepata usajili ambazo zitasaidia kutatua adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipotembelea boma la nyumba ya walimu katika shule ya Msingi Makose.

Naye Emmanuel Nzoka ameshukuru serikali kupitia kwa mbunge kwa kutengeneza barabara na kuwa katika hali nzuri katika majira yote ya mwaka.

“Tulikuwa kisiwani kutokana na barabara kuharibika kutokana na maji ya mvua hivyo kushindwa kupitika katika majira ya masika.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news