YALIYOSISIMUA 2022:Picha bora zaidi iliyovuta hisia katika sanaa na burudani


Miongoni mwa picha ambazo mwaka huu zilivuta hisia kubwa zaidi kutoka katika tasnia ya burudani Tanzania ni baada ya Kajala Masanja ambaye alikuwa mpezi wa Rajab Abdul Kahali (Harmonize) mwezi Septemba, wakati penzi lao likiwa limekolea kuposti picha akiwa na Harmonize katika mavazi rasmi kuonesha kwamba walikuwa wanatoka sehemu kama kanisani.

Kajala kwenye Insta Stories zake aliposti video wakicheza wimbo na Harmonize na kufuatisha kwa maneno kwamba hiyo ilikuwa baada ya kutoka kanisani.
 
“Baada ya kutoka kanisani mimi na kijana wangu,” Kajala alieleza huku Harmonize akimshukuru Kajala kwa kumbadili kutoka kuwa kijana mtoro hadi kuwa kijana mzuri. “Mashallah mtoto wa Kisukuma, ahsante kwa kumfanya kijana mtoro kung’aa tena,”Harmonize alisema. 
 
Hata hivyo, penzi la wawili hao halikuweza kudumu kama ilivyokuwa maombi na matarajio ya Watanzania wengi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news