CEO mpya Simba SC aja na mipango thabiti

NA DIRAMAKINI

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba, Imani Kajula ameweka wazi mipango ya utendaji wake mbele ya wanachama katika Mkutano Mkuu baada ya kupewa jukumu hilo muhimu.

Kajula amesema jambo la kwanza atakalofanya ni kuhakikisha anaiunganisha klabu kuanzia Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti, wanachama mpaka mashabiki.

Katika siku yake ya kwanza ofisini ambayo itakuwa Januari 30, 2023 Mtendaji Mkuu huyo amepanga kwenda kuwatembelea wadhamini wao.

“Tunataka tushinde, lazima kujenga timu bora, lakini kazi ya pili ni kujenga taasisi imara na endelevu hata nisipokuwepo kuwe na mtu mwingine wa kuendeleza, lakini pia kujenga chapa imara na kuongezea mapato na kingine ni kuongeza wadhamini wengine ambayo ni moja ya majukumu yangu.

“Pia lengo ni kuifanya klabu kuwa na fedha zakutosha, ili kufanya mambo yetu kwa urahisi,” amesema Kajula.

Mtendaji huyo pia ameeleza kuwa mikakati yake mingine ni kuhakikisha Simba inafanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kama ilivyofanya timu yao ya wanawake ‘Simba Queens’ mwaka jana, hivyo ni lazima waekeze nguvu katika kuandaa programu maalumu zitakazowasaidia kufikia malengo hayo.

Kajula amesema lengo lao msimu huu ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu na kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wanataka kufika robo fainali au zaidi ya hapo, wakati kwa  Simba Queen wanataka  kufanya vizuri zaidi Afrika na kuboresha timu za vijana.


Mtendaji Mkuu huyo amesema miongoni mwa vitu atakavyovisimamia ni:

­čö╣ Kuhakikisha wakati mwingine watafanya Mkutano Mkuu wa kitkenolojia utakaowahusisha wanachama wote nchi nzima.

­čö╣Kujenga timu imara kwa ajili ya mataji. Kuboresha benchi la Ufundi.

­čö╣Kuimarisha chapa ya klabu na kuitumia vizuri kuwaongezea kipato.

­čö╣Kusimamia ujenzi hosteli za kisasa na tayari mchoro umekamilika.

­čö╣Kuboresha Sherehe za Simba Day

­čö╣Kuunganisha matawi kote nchi nzima

Post a Comment

0 Comments