Try Again:Simba SC hakuna unyonge tena, tumejiimarisha

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewaahidi wanachama, wapenzi na mashabiki kuwa kikosi kinaendelea kuboreshwa na mataji ambayo waliyapoteza watayarejesha.

Try Again amesema, msimu huu watapambana kuhakikisha wanashinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC pamoja na michuano ya Azam Sports Federation Cup ambayo wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa, hakuna unyonge tena mipango ni thabiti na kila kitu kinaenda sawa huku akigusia suala la usajili la msimu ujao kuwa utakuwa mkubwa na bajeti yake tayari imetengwa.

Pia Try Again amethibitisha kuwa, msimu huu watashiriki michuano ya Super Cup kwa kuwa ni miongoni mwa timu bora 10 barani Afrika ambazo ndio zenye vigezo vya kushiriki na hapa nchini watakuwa timu pekee.

“Tutapambana kuchukua ubingwa wa Ligi pamoja na FC kwa uwezo wa Mungu, na kila kitu kimepangwa na tutafanikiwa.

“Pia kipekee ninamshukuru mwekezaji Mohamed Dewji kwa kuendelea kutoa pesa kwa ajili ya kuiboresha timu. Mo anahitaji pongezi kubwa na kwa kiasi kikubwa ameifikisha Simba hapa ilipo.

“Ninamshuku Mtendaji Mkuu aliyemaliza muda wake, Barbara Gonzalez kwa utendaji wake uliotukuka, amefanya kazi kubwa na tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya.

“Tutashiriki Super Cup na itakuwa timu pekee kutoka ukanda huu tupo nafasi 10 kwa ubora Afrika pia hayo ni mafanikio makubwa,”amesema Try Again.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news