Wanafunzi mbaroni kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi mkoani Arusha, limefanikiwa kuwakamata wanafunzi wawili wa Chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanafunzi wa chuo hicho kwa njia ya mtandao.

Akitoa taarifa hiyo Januari 29, 2023 Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Justine Masejo amewataja waliokamtwa kuwa ni Efron Isaya (32) na Cosmas Robert (26), wote wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo hicho.

Amesema, Januari 21 mwaka huu saa 11 jioni katika Chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI), kilichopo Wilaya ya Arumeru kuliripotiwa tukio la unyanyasaji wa kijinsia mwanafunzi wa chuo hicho, (jina limehifadhiwa) kwa njia ya mtandao na wanafunzi wenzake.

ACP Masejo amesema, baada ya kupata taarifa hiyo jeshi hilo lilianza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata wanafunzi hao wawili.

Masejo amesema bado jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news