Huu ni mwaka wa sala na kazi, tukatende kazi tukiwa na hofu ya Mungu-Waziri Dkt.Mabula

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt.Angeline Mabula amewatakia Watanzania heri ya mwaka mpya 2023 na kuwataka kutumia mwaka huo kuchapa kazi kwa bidii ili kuliletea taifa maendeleo.
Dkt.Mabula alitumia maadhimisho ya mwaka mpya usiku wa kuamkia Januari Mosi,2023 nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kwa kutoa rai kwa watanzania wote kuutumia mwaka wa 2023 kufanya kazi kwa bidii huku wakiwa na hofu ya Mungu.

"Rai yangu katika mwaka huu mpya wa 2023 ni mwaka wa sala na kazi, tukatende kazi tukiwa na hofu ya Mungu tukatumikie Watanzania taifa linatutegemea kila la kheri watanzania wote Mungu awabariki sana,"amesema Mheshimiwa Dkt. Mabula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news