JE? WAANDISHI WA HABARI WALIPWE MADAI YAO WAKIWA WAMEKUFA

NA LEORNAD MAPULI

MWAKA jana nikiwa katika likizo yangu ya mwaka na kupenda kwangu kuzima simu kwa maana ya kupumzika nilikutana na habari mbaya ya kugongana magari na kusababisha vifo vya watu 14 kule Mwanza.

Miongoni mwao wakiwemo rafiki zangu wandishi wa habari niliofanya nao kazi akiwemo mdogo wangu Antony Chuwa na dada yangu Husna Mlanzi,niliumia.

Wakati ninaanza kazi Star Tv,Chuwa ndiye alinipokea na nikakaa nae ofisi moja, kabla hajafukuzwa kazi kwa sababu ya kudai haki zake na kuwa mwiba.
 
Zinazohusiana
Mwaka 2018,Chuwa aliondolewa kazini kwa sababu ya yeye na wengine wachache kufungua kesi ya madai mahakamani,kudai haki zao,kampuni haikupenda,iliona kama imedhalilishwa mno, lakini ukweli ni kwamba jamaa walichoka kuishi maisha ya shida ili hali wakimtazama mwenye kampuni si mtu wa shida bali wa mazoea.

Januari 12,pale uwanja wa Nyamagana,miili mitano ukiwemo wa Chuwa na Husna,iliagwa,Serikali iliwakilishwa na Nape Nnauye,Waziri mwenye dhamana,tena akiwa na siku mbili tangu kuapishwa kama waziri katika Serikali ya mama yetu Samia,baada kusugua benchi wakati wa JPM.

Katika hotuba yake,Nape pamoja na pole,aliagiza marehemu Chuwa na Husna walipwe madeni yao ndani ya siku saba,waliyokuwa wakidai kampuni ya Sahara Media Group,na yalilipwa ndani ya siku mbili.

Maana yake ni nini? Ni kwamba Serikali ikiamua kupambania watu wake inaweza! sasa najiuliuliza,Nape alilegea wapi baada ya pale kuwapambania wanahabari? Au anasuburi tena mpaka wafe?.

Ninapondelea na mfululizo wa simulizi zenye nia njema kwa watu mnaowafahamu,sitaki nimsumbue mama yangu Samia…nchi ni kubwa,na ndio maana ana wasaidizi, aliowapa imani ya kumsaidia,mstake kila kitu tumpelekee personally,ana mambo mengi na ndio maana ana wasaidizi. Sahara hawapo juu ya sheria kiasi cha watu kulia kila siku bila msaada,ni wananchi wa nchi hii.WASAIDENI.

Haiwezekani nchi inasisitiza ulipaji kodi kwa maendeleo,halafu kuna wahuni wanakwepa kodi kwa ujeuri kana kwamba wanaishi Burkinafaso,kumbe wapo Bongo na hawafanywi kitu,na pesa wanazo,wakati serikali inapambana na machinga wa Kariakoo wanunue EFD halafu wao hawalipi mishahara ya watu zaidi ya 400 ambao kila mshahara wangechangia asilimia 18 kama kodi.

Marehemu Chuwa pamoja na uwezo mkubwa kitaaluma na talent yake,alidhoofishwa na kutolipwa,akapata stress, akaishia kuwa mla ulabu alewe asahau shida zake, hali mbayo baba yake najua mpaka leo anaamini mwanae alikufa kwa kukosa dira ya maisha iliyosababishwa na uhuni wa Sahara Media Group, na sidhani kama tena ana moyo wa kusomesha mtoto uandishi wa habari maana anaogopa kupoteza pesa.

Husna na Chuwa walilipwa madai yao baada kifo,je? Tusubibiri mpaka watu wafe ndio tuwapambanie au tuendelee kupambana wakiwa hai ili wao na vizazi vyao watukumbuke? Kaka Nape,mama yangu Ndalichako,msaidieni rais,kakupeni nafasi hizo kurahishisha kazi zake,anafanya kazi kubwa,wenye akili tunamuelewa,achana na wanasiasa ambao kila mmoja ana maslahi yake.

Endeleeni kupumzika rafiki zangu Chuwa na Husna,lakini somo mlilotuachia hatuna budi kuliishi,wala injili mlioiacha lazima tundelee kuihubiri ili nasi tukifa mtupokee kwa bashasha.

Pumzikeni kwa Amani,tupo nyuma tunafuata.

Chuwa na Husna walipotez maisha Januari 11,2022.Ijumaa ntakupeni simulizi ya baba yangu Samadu Hassan alivyoniaga newsroom saa moja jioni,na kesho yake asubuhi nikaamushwa na taarifa ya kifo chake cha ghafla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news