Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa aguswa na REA inavyoimarisha uhusiano mzuri na wafanyakazi

NA VERONICA SIMBA-REA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), ngazi ya Taifa, Herry Mkunda ameipongeza Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kujenga uhusiano mzuri baina yake na wafanyakazi katika kuhakikisha wanatekeleza kwa tija malengo ya taasisi kwa manufaa ya Watanzania.
Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Herry Mkunda akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Baraza hilo liliketi jijini Arusha, Januari 20, 2023 kujadili Bajeti ya matumizi ya REA kwa Mwaka 2023/24.

Ametoa pongezi hizo leo Januari 20, 2023 jijini Arusha, wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la REA, lililoketi kujadili Bajeti ya matumizi ya Wakala hiyo kwa Mwaka 2023/24.

Akitolea ufafanuzi chimbuko la pongezi zake kwa REA, Mkunda alibainisha kuwa wafanyakazi katika baadhi ya Taasisi huwa hawashirikishwi na Menejimenti kwa kiwango kinachotakiwa katika kujadiliana na kupanga kwa pamoja namna nzuri ya kutekeleza malengo ya Taasisi ili kupata matokeo chanya suala ambalo ni tofauti kwa REA kutokana na ushirikiano uliopo baina ya pande hizo mbili.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakishiriki kikao cha Baraza hilo kilichoketi jijini Arusha, Januari 20, 2023 kujadili Bajeti ya matumizi ya REA kwa Mwaka 2023/24.

“Kwahiyo niwapongeze Menejimenti ya REA pamoja na Wafanyakazi kwa kukubali kukutana pamoja na kukaa Meza moja kujadiliana kwa lengo la kuhakikisha kwamba malengo ya Taasisi yanatekelezwa kikamilifu na kwa tija,” amesema Mkunda.

Aidha, Katibu Mkuu huyo wa TUGHE Taifa, amesema ni jambo la kujivunia na kupongezwa kwa REA kuwa na zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi wake ambao ni wanachama wa TUGHE.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Aziz Abbu akizungumza wakati wa kikao cha Baraza hilo kilichoketi jijini Arusha, Januari 20, 2023 kujadili Bajeti ya matumizi ya REA kwa Mwaka 2023/24.

Pamoja na pongezi hizo, Mkunda amewaasa wafanyakazi wa REA kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidi ili kuwezesha kufikia malengo ya Mwajiri ambaye ni Serikali ambaye anataka Watanzania wapate huduma njema katika sekta ya nishati vijijini.
Amesema katika baadhi ya Taasisi, wafanyakazi wamekuwa wakichangia kutofikiwa malengo ya Taasisi kutokana na vitendo vya ubadhirifu pamoja na uvivu hali ambayo inasababisha kurudisha nyuma jitihada za Mwajiri.

“Niwaombe tushirikiane kwa pamoja katika mipango na utendaji kazi ili kuhakikisha tunafikia malengo ya Mwajiri,” amesisitiza Mkunda.
Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma, Samwel Nyungwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Baraza hilo liliketi jijini Arusha, Januari 20, 2023 kujadili Bajeti ya matumizi ya REA kwa Mwaka 2023/24.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakishiriki kikao cha Baraza hilo kilichoketi jijini Arusha, Januari 20, 2023 kujadili Bajeti ya matumizi ya REA kwa Mwaka 2023/24.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA ambaye kwa nafasi yake ndiye Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la REA, Mwakilishi wake katika kikao hicho Musa Muzze alimhakikishia Kiongozi huyo wa TUGHE Taifa kuwa Menejimenti ya REA imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wafanyakazi wanashirikishwa ipasavyo katika kila jambo linalohusu taasisi.
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mussa Muze, akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza hilo kilichoketi jijini Arusha, Januari 20, 2023 kujadili Bajeti ya matumizi ya REA kwa Mwaka 2023/24.

“Tofauti na baadhi ya maeneo mengine, kwa upande wa REA, Menejimenti imekuwa mstari wa mbele katika kuwathamini wafanyakazi. Mfano mzuri ni kwamba hata uanzishwaji wa Baraza la Wafanyakazi REA, Menejimenti ndiyo ilihamasisha na kuhakikisha suala hilo linafanikiwa,”amefafanua Muzze.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Swalehe Kibwana, akichangia maoni wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi. Kikao hicho kiliketi jijini Arusha, Januari 20, 2023 kujadili Bajeti ya matumizi ya REA kwa Mwaka 2023/24.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la REA, Swalehe Kibwana ameushukuru Uongozi wa Wakala hiyo kwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa wafanyakazi katika masuala ya kazi na hata masuala yanayowahusu wafanyakazi wenyewe.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Herry Mkunda, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mussa Muze na Katibu wa Baraza hilo Aziz Abbu, wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi. Kikao hicho kiliketi jijini Arusha, Januari 20, 2023 kujadili Bajeti ya matumizi ya REA kwa Mwaka 2023/24.

“Sisi tuna bahati. Mojawapo ya bahati tulizopata ni ushirikishwaji, jambo ambalo kwakweli hatuna budi kutoa shukrani kwa Uongozi,” amesisitiza Kibwana.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma, Samwel Nyungwa ambaye ameungana na Katibu Mkuu Taifa kuipongeza REA kwa ushirikiano mzuri katika kutekeleza majukumu ya Taasisi kwa manufaa ya Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news