KILO 399.28 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekamata jumla ya kilo 399.28 za dawa za kulevya aina ya bangi katika Kitongoji cha Sokoni, Kijiji cha Chogoali,Kata ya Iyogwe,Tarafa ya Gairo Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), ukamataji huo umefanyika kufuatia operesheni iliyofanywa na mamlaka mkoani humo tarehe 22 Disemba mwaka 2022 ambapo watu wawili wanashikiliwa kuhusika na usafirishaji wa kiasi hicho cha bangi.

Aidha,watumia hao wamekutwa na bunduki mbili aina ya gobore zenye namba MG-188 na MG-148 pamoja na ngozi ya mnyama anayedhaniwa kuwa ni Kakakuona.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inaendelea kufanya operesheni katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha inadhibiti uzalishaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news