KMC FC yajiandaa kuikabili Mtibwa Sugar

NA DIRAMAKINI

WACHEZAJI wa Timu ya KMC FC wamereja kambini na kuanza maandalizi kuelekea katika mchezo unaokuja wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Januari 13, 2023 katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni imeingia kambini ikijiandaa na Mtibwa Sugar ambapo itakuwa ugenini na Kocha Mkuu, Thierry Hitimana ambaye pia alikuwa Rwanda kutokana na kufiwa na mdogo wake pia ameingia na kuanza kukinoa kikosi hicho.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC,Christina Mwagala ikielezea kuhusiana na maandalizi hayo.

"Aidha, katika kikosi hicho cha wana Kino Boys wachezaji wote wamerejea huku ikiwakosa wachezaji saba kutokana na sababu mbalimbali ambao ni Sadalah Lipangile, Ibrahimu Ame, Matheo Anton, Steve Nzingamasabo pamoja na Ismail Gambo ambapo wote ni kutokana na changamoto za kifamilia huku Emmanuel Mvuyekure na Hance Masoud wakiendelea kupatiwa matibabu kutokana na majeraha ya muda mrefu.

"Tumeanza mazoezi baada ya mapumziko mafupi ambayo tuliwapa wachezaji katika kipindi hiki ambacho timu zipo kwenye mapumziko kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, kikubwa tunakwenda kwenye mchezo mgumu ambao tutakuwa ugenini na ndio mana tumekuwa na muda mfupi wa kupumzika, lengo likiwa kujiandaa vizuri kwa ajili ya kupata matokeo chanya.

"Tutakuwa na mchezo mgumu ambapo ukizingatia tutakwenda tena ugenini baada ya kutoka kupoteza dhidi ya Ihefu, Januari 3, mwaka huu, lakini tunafurahi kuwa wachezaji wetu wamerudi kwenye viwango vizuri hata kwenye mazoezi wanafanya wakiwa na ari na morali nzuri ambayo inaleta taswira njema kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar,"amefafanua.

KMC FC inakwenda kwenye mchezo wa mzunguko wa 20 ikiwa kwenye nafasi ya tisa mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na jumla ya alama 22.

Aidha,mashabiki na Watanzania wote ambao siku zote wamekuwa wakiisapoti pindi inapokuwa uwanjani wameombwa kuendelea kufanya hivyo, kwani watakwenda kupambana katika michezo iliyobaki na kufanya vizuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news