Kocha Mkuu Roberto Oliviera asema Simba SC itafika Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam imemtambulisha Mbrazil, Roberto Oliviera (Robertinho) kuwa kocha wake mpya mkuu.

Utambulisho huo umefanyika Januari 3, 2023 ambapo amesema, siku zote anawaza vitu vikubwa na malengo yake ni makubwa ikiwemo kufika Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Robertinho ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha klabu hiyo amesema, watu wengi wamekuwa wakifikiria kuhusu hatua ya makundi, lakini ukiweka mipango mizuri hata fainali inawezekana.

Kuhusu ubingwa wa Ligi ya Kuu ya NBC Tanzania Bara, Robertinho amesema yeye ni mshindani na anaamini katika mipango thabiti, hivyo kila kitu kinawezekana.

“Nimewahi kuwa mchezaji kabla ya kuwa kocha, siku zote ninaamini katika mipango mizuri. Ukiwa na mipango mizuri unaweza kufika nusu fainali mpaka fainali hilo linawezekana pia nikiwa hapa Simba.

“Wakati niko Vipers tulipokuwa tunaenda kukutana na TP Mazembe wengi waliamini ulikuwa mwisho wetu, lakini tulikuwa na mipango mizuri mpaka tukafanikiwa kuwatoa,”amesema Robertinho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu amesema, kitu kilichotuvutia kwa Robertinho ni ubora na uzoefu wake kwa soka la Afrika Mashariki kwa hiyo wanaamini atawafikisha wanapopataka.

“Robertinho ni kocha mwenye wasifu mkubwa nasi tuna malengo makubwa ndiyo maana tumemchukua, ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika Mashariki hilo pia limetuvutia,”amesema Mangungu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news