Mheshimiwa Othman:Zipo fursa nyingi za kiuchumi na uwekezaji kati ya Zanzibar, UAE

NA DIRAMAKINI

IMEELEZWA kwamba zipo fursa nyingi za kiuchumi na uwekezaji zinazoweza kutumika kwa ushirikiano na kuchangia kuleta maendeleo makubwa kati ya Zanzibar na nchi za Falme za Kiarabu (UAE).
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani jijini Zanzibar alipokutana na kuzungunza na Balozi Mdogo wa Nchi za Falme za Kiarabu, Bw.Saleh Alhemeiri kuhusiana na ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

Mhe. Othman amesema kwamba, nchi kwa kuwa zinao uhusiano mkubwa wa kijamii hivyo fursa za mashirikiano katika maeneo ya uchumi, wa bluu, utamaduni, uvuvi, Kilimo na biashara katika sekta ya huduma ya usafiri wa anga.

Amesema kwamba, Zanzibar inaweza kuutumia na kufaidika na uzoefu mkubwa uliopo katika nchi hizo ili kusaidia pamoja na mambo mengine kujenga uwezo wa Zanzibar katika maeneo mbali mbali kwenye sekta hizo na kuweza kuwa na tijha kubwa kimaendeleo.

Ameongeza kwamba sekta ya uchukuzi wa anga hivi sasa inamuelekeo wa kuwa sekta kubwa na tegemeo muhimu la kiuchumi inayoweza kusaidia Zanzibar kuweza kupiga hatua kimaendeleo.
 
Naye Balozi Mdogo wa UAE Bw. `Saleh Alhemeiri, asmesema kwamba UAE ipo tayari kuisaidia Zanzibar katika maeneo mbali mbali ya sekta hizo ili kuendelea kujenga uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Amesema kwamba nchi hiyo wanaweza kusaidia pia kutoa mafunzo kwa vijana kutoka Zanzibar ili kuisaidia Zanzibar kuwa kituo muhimu katika sekta ya huduma ya usafiri wa Anga.

Wakati huo huo Mhe. Othman amekutana na ujumbe Watendaji wa Taasisi kutoka Ofisi ya Rais ya Ufuatiliaji ,usimamizi wa Utendaji Serikalini na kuwaeleza kwamba taasisi hiyo inakazi kubwa ya kusaidia kunyanyua na kutimiza matumaini ya wananchi hasa wanyonge kwa kuwepo na kuimarika utolewaji wa huduma za kijamii kama matarajio ya wananchi yalivyo.

Mhe. Makamu amesema kwamba taasisi hiyo ni nyenzo muhimu katika kufikia matarajio ya kweli na matumaini mazuri ya wananchi iwapo watendaji hao wataangalia, kuanisha na kuyafanyia kazi maeneo mbali mbali muhimu yatakayosaidia kunyanyua uchumi na maendeleo ya Zanzibar.

Amesema kwamba, yapo maeneo mengi yanayohitaji kufanyiwa kazi ili kusaidia ipasavyo nchi katika kunyanyua matumaini na matarajio ya wananchi wa Zanzibar hasa kwenye kufikia upatikanaji wa huduma bora za kijamii na maendeleo kwa jumla. 
 
Naye Kiongozi wa ujumbe huo ambaye ni naibu mtendaji Mkuu wa Taaisi hizi Ndugu Josphine Kimaro amesema kwamba taasisi hiyo imeundwa katika kusaidia utekelezaji wenye tija kwa maeneo ya vipaumbele vya maendeleo vilivyowekwa na serikali ikiwemo uchumi wa bluu, miundombinu,huduma za jamii kama afya , umeme na maji sambamba na kuwafahamisha wananchi kuhudu juhudi za serikali kwenye hatua za utekelezaji wa mambo mbali mbali yalivyopfikiwa.

Post a Comment

0 Comments