Sekta ya Kilimo kukua kwa asilimia 10 ifikapo 2030-Rais Dkt.Samia

DAVOS-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema sekta ya kilimo nchini inatarajiwa kukua kwa 10% ifikapo mwaka 2030 ukilinganisha na ukuaji wa sasa wa takriban 3.6%.
Rais Samia amesema Tanzania imetengeneza fursa za kitaifa kwa ajili ya mabadiliko ya mfumo wa chakula unaotarajia kuongeza uzalishaji wa chakula, kuimarisha maisha ya watu na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akichangia kwenye mada inayohusu masuala ya chakula ‘Food Action Partnership: Investing in Greater Resilience’, ikiwa mkutano mwingine wakati wa Jukwaa la Uchumi Duniani, Uswizi Rais Samia alizungumzia dira ya mabadiliko ya kilimo Tanzania.Katika kudhibiti mfumo endelevu wa chakula nchini, Rais Samia amesema jitihada kadhaa zimefanyika, ikiwemo kuanzisha mradi kwa ajili ya vijana huku wakiendelea kuimarisha ukuaji wa shoroba za kilimo.

Jitihada nyingine zilizofanyika kuanzia mwaka huu wa fedha ni pamoja na kuongeza bajeti ya kilimo mara 4 ukilinganisha na ile iliyopita. Aidha, Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika mwezi Septemba kudhihirisha maendeleo hayo.

Mdahalo huo ulihudhuriwa na zaidi ya Viongozi 50 kutoka Afrika, Asia, Ulaya na Marekani kwa nia ya kuongeza kasi ya ushirikiano na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kila nchi.
Wachangiaji wakuu katika mdahalo huo mbali na Rais Samia walikuwa Rais Gustavo Petro wa Colombia, Tran Hong Ha, Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam na Bw Alvaro Lario, Rais wa Wakfu wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Roma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news