Rais Dkt.Mwinyi amteua Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA)

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 16, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo umeanza Januari 10, 2023.

"Kufuatia kufutwa kwa Sheria ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ya mwaka 1996 na kutungwa Sheria ya Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ya mwaka 2022.

"Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA),"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndugu Yusuph Juma Mwenda alikuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news