Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewateua viongozi mbalimbali.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 20, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Samora John Chacha kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

Ndugu Chacha kabla ya uteuzi huo uliofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alikuwa ni mfanyakazi wa sekta binafsi.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Adil Fauz George kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Uratibu wa Shughuli za Utalii katika Kamisheni ya Utalii. Kabla ya ndugu Adil kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alikuwa ni mfanyakazi wa sekta binafsi.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Yakout Hassan Yakout kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, ndugu Yakout ni Katibu Mkuu mstaafu.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Ali Saleh Mwinyikai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Magazeti. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndugu Ali ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Bibi Safia Ali Rijaal kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar. Bibi Safia ni mstaafu katika utumishi wa umma. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo unaanza Januari 20, 2023.

Sita, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Ussy Khamis Debe kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya uteuzi wa ndugu Ussy alikuwa Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar na uteuzi wake umeanza Desemba 30,2022.

Post a Comment

0 Comments