Rais Dkt.Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali,Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa - Muhimbili. 

Dkt. Mkondya ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Justine Peter Mwandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC). 

Bw. Mwandu ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Reinsurance (TANRE).

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. 

Bw. Mwakapeje alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria. Bw. Mwakapeje anachukua nafasi ya Bw. Casmir S. Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake tarehe 07 Januari, 2023.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bi. Fatma Mohamed Abdallah kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Puma Energy Tanzania. 
 
Bi. Abdallah ni Meneja wa Kampuni ya Puma Energy jijini Geneva, Uswisi. Aidha, Bi. Abdallah anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza muda wake.

Sita, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. David Zacharia Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). BW. Kafulila ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mstaafu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 5, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bi.Zuhuru Yunus, teuzi hizi zinaanza mara moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news