Rais Dkt.Samia atengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri Nne

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi wa Mkuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri nne.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Januari 24, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Dkt. Samia ametengua uongozi wa BW. Reuben Ndiza Mfune ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.

Rais Dkt. Samia amemtengua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Bw. Msongela Nitu Palela

Amemtengua Bw. Michael Augustino Matomora aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Singida;

Amemtengua Bw. Linno Pius Mwageni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Shinyanga; na

Aidha amemtengua Bw. Sunday Deogratius Ndori, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Njombe.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, utenguzi huu ulianza tarehe 22 Januari, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news