Serikali yatangaza habari njema kwa watendaji wa kata

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amesema, pikipiki zipatazo 916 zitagawiwa kwa watendaji wa kata ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Waziri Kairkuki ameyasema hayo Januari 20, 2023 wakati alipomuwakilisha Makamu wa Rais katika hafla ya kuufahamisha umma mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Mkoa wa Dodoma.

Akijibu ombi la Mtendaji wa Kata ya Uhuru katika Jiji la Dodoma,Christina Mpete kuhusu uwezeshaji wa vyombo vya usafiri hususani ni pikipiki kwa watendaji hao ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo,Mhe. Kairuki amesema;

“Niwape habari kuwa ombi hilo limekuja wakati muafaka ambako Serikali imeshanunua pikipiki hizo na zitagawiwa wakati wowote kuanzia sasa na tunaenda kwa awamu kwa sasa watendaji 916 watapatiwa pikipiki hizo,"amefafanua Waziri Kairuki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news