Rais Dkt.Samia awaapisha viongozi aliowateua

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo Januari 9, 2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo.Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya Hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leoRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news