TARURA:Tunachunguza taarifa za Daraja la Sasenga mkoani Songwe kubomoka

NA DIRAMAKINI

KUTOKANA na video inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kubomoka kwa Daraja la Sasenga linalounganisha vijiji vya Ikumbilo na Chitete katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe lililokuwa linaendelea kujengwa, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wamesema wanaendelea kufanya uchunguzi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 8, 2023 na Geofrey A.Kazaula ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, TARURA.

"Tunapenda kuwafahamisha kuwa, suala hili linafanyiwa uchunguzi na endapo itabainika kuna uzembe wowote wa kiutendaji uliofanyika katika usimamizi au upande wa Mkandarasi hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wahusika na upande wa Mkandarasi kulingana na mkataba;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news