Chanzo cha ajali iliyoua abiria 12,kujeruhi 63 chatajwa

NA DIRAMAKINI

MWENDO kasi umetajwa kuwa, chanzo kikuu cha ajali iliyosababisha vifo vya watu 12 na kujeruhi 63 katika Kata ya Pandambili Kijiji cha Silwa wilayani Kongwa karibu na Barabara ya Dodoma kwenda Morogoro.
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Februari 9, 2023 wilayani Kongwa mkoani Dodoma ikihusisha lori lenye namba za usajili T 677 DVX na basi la abiria la Kampuni ya Frester lenye namba za usajili T 415 DPP lililokuwa likitokea Bukoba kwenda jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Awadh Haji ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa basi kutaka kulipita gari la mbele bila ya kuchukua tahadhari na kugongana na lori lililokuwa limebeba saruji.

Mheshimiwa Rosemary Senyamule ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa, ajali hiyo imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 12 ambapo kati yao ni wanaume wanane, wanawake wanne na majeruhi 63 huku wanaume wakiwa 40 na wanawake 23.

“Serikali ilikuwa na nia njema ya kuruhusu vyombo vya usafiri kutembea usiku, lakini sasa baadhi ya madereva wanaanza kutozingatia sheria za usalama barabarani, tutaendelea kuwachukulia hatua kali,"amesema RC Senyamule.

Aidha, majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma na Kituo cha Afya Gairo mkoani Morogoro. Pia, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mkoa wa Morogoro na majeruhi wawili wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo.

"Nawapa pole wafiwa waliopoteza jamaa zao katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Silwa, Dodoma usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2023 na kusababisha vifo vya watu 12. Mungu awarehemu Marehemu wote. Naviagiza vyombo vya dola kuongeza usimamizi wa sheria za usalama barabarani;
Tazama orodha ya majina hapa chini majeruhi waliopo Morogoro;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

9 Comments

  1. Vifo 12
    Majeruhi 63
    Jumla 75

    Haya mabasi yanajaza abiria kupitiliza, hatuna basi za mikoani inaweza kubeba idadi hiyo

    Halafu njiani Kuna check points nyingi zisizo na tija

    ReplyDelete
  2. Usiku wanajaza Sana hadi kwenye zile koridor Mana wanajua askari usiku hawakagui

    ReplyDelete
  3. Karibia mabasi mengi ya mikoani watu wanasimama utakuta wengine wanachuchumaa

    ReplyDelete
  4. Kweli kabisa wanasema wanaongeza Posho zao

    ReplyDelete
  5. Wanaweka kwenye koridi vigoda magari mengi jamani wakuwabana ni Dereva na Kondakta wanagawana pesa za vigoda na vindoo vidogo abiria hana sauti kabisa wakomeshwe wahusika dereva na utingo wake na abiria tupige simu walizotuwekea ndani ya bus tena nyuma ya dereva

    ReplyDelete
  6. Kama viongozi wanasikia,tupo wazalendo tunaoweza kusafiri kwenye hayo mabasi na tukawaripot inapotokea.

    ReplyDelete
  7. Abiria wanateseka na hawana la kufanya.inaumiza sana

    ReplyDelete
  8. Hata safari za usiku zipigwe marufuku ikifika saa kumi ba mbili au linapoishia giza magari yasimame mpaka saa 11 alfajiri atakaye vunja masharti hayo achukuliwe hatua jamani ajali nyingi ni usiku hata za daa Moro sikome usiku

    ReplyDelete
  9. Hii saa 1 mpaka saa 4 eti Dar Moro aaa mmm zisiwepo tutazoea tu

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news