Serikali yaagiza madereva hawa wafutiwe leseni

NA DIRAMAKINI

NAIBU Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ametoa maelekezo kwa Makamanda wa Mikoa kuwafutia na kuwanyang'anya leseni madereva hatarishi ambao wamekuwa hawafuati na kuzingatia sheria za usalama barabarani, licha ya elimu ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikitolewa na Jeshi la Polisi.
Sagini amesema hayo wakati alipowajulia hali baadhi ya majeruhi wa ajali iliyotokea Februari 9,2023 ambayo imesababisha vifo vya watu 12 na majeruhi 63 mara baada ya basi la abiria la Kampuni ya Frester kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba saruji katika Kijiji cha Silwa Pandambili, Barabara Kuu ya Dodoma-Morogoro.
Akizungumza na majeruhi wa ajali hiyo ambao 25 waliruhusiwa mara baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo na kuruhusiwa kuendelea na safari Sagini amewataka wananchi kuhakikisha wanapaza sauti zao kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya mwendo kasi kwa madereva au wanapoona kusimama kwa safari mara kwa mara kutokana na ubovu wa magari wanayosafiria kwa kupiga namba za simu za Makamanda wa Polisi zilizopo ndani ya mabasi wanayosafiria.
"Wadau wa usafirishaji wakiwemo madereva na sisi abiria wote inapaswa tuguswe na mwenendo wa madereva wetu tukatae na tupige kelele. 

"Pale unapoona dereva anaendesha kwa mwendo hatarishi kataeni kwa sababu mkinyamaza na baadhi mkishangilia wakati mwingine mnakwenda kushangilia yanayopelekea mwisho wetu. 

"Uamuzi wa Dereva yule haukuwa uamuzi kabisa wa mtu mwenye akili za kawaida unaovertake magari mawili yote marefu na mbele mnaona kuna gari inakuja akili za kawaida zinakwambia subiri. Lakini akili zake zikamwambia nenda na abiria mmo ndani yake,”amesema Sagini.
Sagini amewasihi wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri kuwa vyombo hivyo vina masharti yake, kuna viwango vya spidi ya kutembea lakini pia kama unataka kupita gari nyingine lazima uwe na tahadhari ya kutosha kwani dereva aiyesababisha ajali hakuwa na tahadhari ya kutosha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. jamani madereva tuweni makini tunapokuwa barabarani`

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news