Rais Dkt.Samia afanya uteuzi TFRA, TANAPA

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua, Bw. Antony Diallo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA). Bw. Diallo anachukua nafasi ya Prof. Anthony Mshandete ambaye amemaliza muda wake.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 14, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus ambapo uteuzi huu umeanza Februari 9, 2023.

Pia Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Marwa Waitara kwa kipindi kingine kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi Tanzania (TANAPA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Marwa Waitara umeanza Februari 13, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news