NA DIRAMAKINI
KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Roberto Oliviera (Robertinho) amesema, walikosa bahati katika mchezo wao dhidi ya Horoya na hilo limesababisha kupoteza ugenini kwa bao moja.
Mtanange huo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya uliopigwa Februari 11, 2023 katika Uwanja wa Jenerali Lansana Conte nchini Guinea.
Robertinho amesema, walipoteza nafasi tatu za wazi walizotengeneza ambazo wangetumia hata moja wasingepoteza mchezo huo.
Akizungumzia mchezo ulivyokuwa, Robertinho amesema wenyeji Horoya walikuwa bora kipindi cha kwanza, lakini walivyofanya mabadiliko kipindi cha pili waliishika mechi ingawa hawakuzitumia nafasi walizopata.
“Nadhani hatukuwa na bahati, tumepata nafasi tatu za wazi, lakini tumeshindwa kuzitumia. Wenzetu wamepata moja wameitumia na huo ndio mpira.
“Tunarudi nyumbani kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Raja Casablanca, ninaamini wachezaji wetu wataitumia vizuri kupata ushindi nyumbani,”amesema Kocha huyo.
Aidha, mmchezo wetu dhidi ya Raja Casablanca utapigwa Februari 18, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.