Waziri Dkt.Gwajima awauma sikio wanaume

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum amewataka wanaume nchini kushiriki kikamilifu kupinga mila na desturi zenye madhara ili kutokomeza ukeketaji

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Dkt. Gwajima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji dhidi ya Wanawake yanayotarajiwa kufanyika Februari 6 hufanyika kila mwaka.

Ameyasema hayo jijini Dodoma alipozungumza na Waandishi wa Habari kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kupinga Ukeketaji dhidi ya Wanawake yanayofanyika Februari 6 ya kila Mwaka.

Mhe. Gwajima amesema maadhimisho hayo yanalenga kutokomeza vitendo vya ukeketaji dhidi ya Wanawake na kaulimbiu ya Mwaka huu ni “Wanaume na Wavulana; Tushiriki Kupinga Mila na Desturi zenye Madhara ili kutokomeza Ukeketaji”.

Amesema, kau limbiu hiyo inatambua umuhimu wa wanaume katika kushawishi Wanawake na watoto wa kike kutowafanyiwa ukeketeaji.

"Wanaume inatakiwa kubadilika kwanza ndipo jitihada za kupinga ukeketaji zinaweza kufanikiwa. Takwimu zinaonyesha kuwa ukeketaji nchini bado ni tatizo hali inayotokana na baadhi ya Jamii zetu kuendelea kukumbatia mila na Destpuri zenye madhara na Kuwadhalilisha watoto wa kike,”amesema Dkt.Gwajima.

Dkt.Gwajima amesema, Serikali inaendelea na jitihada za kukabiliana na vitendo Vya ukeketaji kupitia mipango na Mikakati iliyowekwa ikiwemo kutunga na kufanya marekebisho .

“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1997) inasisitiza usawa na heshima kwa binadamu wote, Kutambua na kutathmini utu wa Mtu Pamoja na Kuhakikisha haki mbele ya Sheria.”

Aidha ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika ngazi zote kwa kuandaa Mdahalo wa Wadau wanaotekeleza shughuli za kutokomeza ukeketaji nchini pia kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukeketaji kwa njia ya mikutano ya hadhara, vikao na maandamano.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Asha Vuai amesema Serikali inaendelea na juhudi za kupinga ukeketaji dhidi ya Wanawake na Watoto hasa katika mikoa iliyoathiriwa na ukatili huo akitaja mikoa inayoongoza nchini.

“Mkoa Mikoa inayoongoza kwa ukeketaji ni Manyara (58%), Dodoma (47%), Arusha (41%), Mara (32%) Singida (31%) Tanga (14%), Iringa (8%), Njombe (7%), na Pwani (4%)," amesema Aisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news