Kamati ya Bunge yaridhishwa na ujenzi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Kiwanda cha Uchapaji wa Nyaraka za Serikali

NA MWANDISHI WETU

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imeonesha kuridhishwa na hatua ya ujenzi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Ujenzi wa Kiwanda cha Uchapaji wa Nyaraka za Serikali jijini Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa na wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria walipotembelea kujionea Maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha Uchapaji wa Nyaraka za Serikali.(Picha na OWM).

Hayo yamesemwa Machi 18, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria Mhe. Joseph Mhagama katika ziara ambayo ililenga kujionea kile ambacho kimepangwa kwenye bajeti ya Serikali na kuangalia hatua zilizopigwa, changamoto zilizojitokeza na namna ya utatuzi wake.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akisalimiana na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala Katiba na Sheria walipotembelea Taasisi na Idara zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Ziara hii imetuwezesha kupata uhalisia wa hali jinsi ilivyo, ili iweze kutusaidia wakati wa kupanga bajeti, tuwe na uhalisia wa utekelezaji miradi,"amesema. 

Akizungumzia kuhusu Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Mhe.Mhagama amesema, upo muhimu wa idara hiyo kuwa na mifumo rasmi ya kujisimamia bajeti yake yenyewe (kama wakala) ili isaidie idara hiyo iweze kuingia katika soko shindani. 

Ameongeza kuwa,Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ikiweza kujisimamia katika bajeti yake, itasaidia kuongeza Makusanyo mengi ambayo yanategemewa kutoka katika Idara hiyo. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria Mhe. Joseph Mhagama akizungumza, wakati kamati ilipotembelea kujionea Maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Ujenzi wa Kiwanda cha Uchapaji wa Nyaraka za Serikali.

"Tunachangamoto kubwa sana katika utengenezaji wa nembo ya Taifa,lazima tuwe na mamlaka moja ya kutengeneza nembo ya Taifa na watu wengine wote waipate kupitia katika Ofisi ya Mpiga Chapa wa Serikali,“amesema Mhe. Mhagama.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema anakubaliana na maelekezo ya Kamati. Wizara itatoa taarifa mbele ya Kamati hatua iliyofikia katika kuandaa mabadiliko ya sheria ili kuwezesha Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuwa wakala. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa na wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria walipotembelea kujionea Maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. 

Naye Mhe. Ahmed Ngwali Mjumbe wa Kamati, ameshauri Idara ya Mpiga Chapa Mkuu Wa Serikali kufanyia kazi mapendekezo ya kamati mapema ili iweze kubadilishwa na kuwa wakala.

Awali Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw.George Lugome amesema, utakapokamilika mradi wa Kiwanda cha Uchapaji wa Nyaraka za Serikali itasaidia kuimarika kwa utunzaji wa kumbukumbu ikiwa ni sambamba na kuongeza ajira na kuwa sehemu ya mafunzo kwa watu wanasomea masuala ya uchapishaji. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news