Mifuko 776 ya mchanga yakutwa katika ghala la mbolea

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Kilimo,Mheshimiwa Hussein Bashe ameagiza kukamatwa na kuhojiwa Meneja Masoko wa Kampuni ya mbolea ya Minjingu, Dkt.Mshindo Msolla kwa tuhuma za kukutwa na mifuko 776 ya mchanga katika ghala la kampuni ya mbolea ya Minjingu.

Maagizo ya Bashe yanaenda sambaba na kukamatwa kwa msimamizi wa ghala la mbolea ya Minjingu Mkoa wa Njombe na Meneja wa Kanda wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Michael Sanga kwa tuhuma hizo.

Aidha, imeelezwa kuwa, huenda mifuko hiyo 776 ya mchanga inatumika kuchakachua mbolea inayouzwa na kampuni hiyo. Mheshimiwa Waziri Bashe amesema hiyo ni hujuma ambayo haivumiliki, na atahakikisha wahusika wote wanachukuliwa hatua.

Waziri ametoa agizo hilo baada ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na wale wa kamati ya siasa ya mkoa huo, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mheshimiwa Antony Mtaka kufika katika ghala hilo na kukuta shehena ya mifuko ya mchanga katikati ya mifuko ya mbolea ya Minjingu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news